Duration 8:24

MJUMBE WA (NEC) MKOA MWANZA JAMALI BABU,AHAMASISHA KILIMO CHA ALIZETI NA MHOGO KUWA ZAO LA BIASHARA

226 watched
0
0
Published 9 Mar 2020

Shirika la kimataifa la Kimarekani la utoaji wa elimu kwa wakulima (Gaverst International), kwa kushirikiana na shirika la kutoa elimu ya mazao la mhogo na Alizeti (CAPAFO), yameazisha program maalum ya kuhamasisha mazao hayo kuwa mazao ya biashara kanda ya Ziwa. Kutokana na umuhimu wa kilimo katika serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Uchumi wa Viwanda, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza (NEC) Jamal Babu, amewahamasisha wakulima kujituma kikamiliifu , ili kutekeleza sera hiyo kwa ustawi wa Taifa. Katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kutekeleza sera ya Tanzania ya uchumi wa viwanda, mashirika hayo yameona ipo haja ya kuhamasisha mazao ya mhogo na Alizeti, kuwa kiini cha ukuzaji wa sekta ya uchumi nchini. Gretchen Hopley ni mtaalamu wa masuala ya kilimo wa shirika la Gaverst International la Kimarekani, na Daud Machali ni mkurugenzi wa shirika la kutoa elimu kwa wakulima (CAPAFO) la nchini Tanzania. Hatua ya uhamasisha wa mazao ya mhogo na Alizeti kanda ya Ziwa kuwa mazao ya biashara imefuata, baada ya serikali ya awamu ya tano kujipambanua kuwa sekta ya viwanda ndio itakuwa mwarobaini wa kukuza uchumi wa Taifa, lakini pia pato la mtu mmoja mmoja.

Category

Show more

Comments - 0