Duration 2:4:46

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA SIKU YA JUMAPILI

7 510 watched
0
103
Published 19 Apr 2020

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA SIKU YA JUMAPILI 19/04/2020 SIRI YA WASIYOIJUA MAADUI ZAKO WANAOKUTENDEA MABAYA Luka 18 : 31 - 34 Luka 24 : 44 - 47 Luka 23 : 34 Isaya 44 : 18 Mhubiri 10 : 8 - 9 Luka 18 : 31 - 34 31 Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. 32 Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; 33 nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka. 34 Walakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa. Luka 24 : 44 - 47 44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. 46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Luka 23 : 34 34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. Isaya 44 : 18 18 Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu. Mhubiri 10 : 8 - 9 8 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. 9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. Mhubiri: Mwl. Emilian Katubayemo Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 7